Nilihudhuria 70th (1992) birthday ya Mwalimu. Sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha. Alipokuwa anaondoka, mama mmoja kampa portrait yake aliyechora mama huyo mwenyewe. Akamambia msaidizi wake apokee. Zawadi ya Benz kwa Mzee wetu ikanishtua kidogo.
He exited with honour,
Integrity and candour.
With disarming humility,
And unscarred credibility.
Stay well Prof,
You have saved the honour of profs,
With your humble red IST,
Where others have tarred it,
With their intimidating SUVs.
Prof. Assad akiondoka baada ya kukabidhi ofisi kwa CAG mpya, Charles Kichere leo jijini Dar
> Prof. Assad amemaliza kipindi chake kimoja akihudumu kama CAG na ameondoka huku ukiibuka mjadala mkali juu ya kuondoka kwake
#JFLeo
Thinking aloud on
#endofthinking
. I’m amazed at the huge no of Drs& Profs taking nomination forms for Parliament in the forthcoming Tanzania general elections. What is the reason behind this exodus from the academy? Material benefits?Power?Privilege?Positions?PolSecurity?Fear?
Kwani uchifu ni utamaduni wetu? Makabila mengi hawakuwa na wachifu. Waliwekwa na wakoloni kwa maslahi yao (km Wazanaki). Uchifu ulipigwa marufuku na sheria mnamo 1962. Machifu waliyokuwepo (km Adam Sapi, Fundikira, Kunambi nk) waliingizwa Serikalini katika nyadhifa mbalimbali.
Wasome ili iweje!Siasa haihitaji usomi. Biashara haihitaji usomi.Uelewa wa jamii/duniya hauthaminiki.Huna haja ya kujua historia au hatma kwa sababu unaishi kwa sasa(in the present). Maendeleo hayahitaji usomi;busara inatosha.Chuo hakihitaji usomi-kujipendekeza au kudesa inatosha
Enyi WatuWema
Mnijibu kwa dhati.
Kwa nini
Tusisherehekee Uhuru
Kwa maua, michezo na marashi?
Kwa nini
Tusisherehekee Uhuru
Kwa mikongamano, mikutano na mihadhara?
Kwa nini
Tunasherehekea Uhuru
Kwa gwaride, vifaru na ndege za kivita
Kwa mabomu ya machozi na mabunduki ya kutisha?
Naumia sana nikishuhudia nchi yangu iliyokuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi na udhalilishwaji wa utu wa binadamu-ambao ulikuwa msingi wa mtazamo wa kifalsafa/kisiasa wa Mwa-ikiteleza ktk dimbwi ya lugha ya kibaguzi ya kikabila,kidini, kijinsia na udhalilishwaji wa utu bila aibu
Uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi kwa sababu ni msingi wa uhuru wa binadamu. Ukimyamazisha mtu kujieleza ni kudharau utu wa binadamu.
Kama kupumua ni dalili ya uhai
Basi kujieleza ni dalili ya utu.
Haya hii hapa biographia ya Mwalimu iliyoandikwa na Watanzania na kuchapishwa na Mchapishaji wa Kitanzania. Kuna mengi, mengi ya kujifunza. Sisi tumejitahidi sasa kazi kwenu kutafakari. Kinapatikana TPH bookshop Samora Avenue.
#NyerereBiography
#MwalimuBiography
Rafiki yangu dereva wa teksi
Akanikemea:acha kudadisi
Siasa ni mchezo wa sarakasi
Imejaa uzushi
Mie mwananchi
Sio mwenyenchi
Haki yangu ni kupiga kura
Sio kumchagua atakayeenda kula
Wenyenchi huchaguana
Wao kwa wao na vipenzi vyao
Wananchi hubaguana
Wao kwa wao kwa makabila yao
Pamoja na kushirikiana na sekta binafsi, huwezi kuwaingiza wafanyabiashara jikoni wakupikie chakula cha umma!
Sekta ya umma na sekta binafsi hazilinganiki. Ni kweli huwezi kuendesha biashara kama idara ya serikali; pia ni kweli huwezi kuendesha serikali kama kitengo cha biashara.
Kinyume cha HAKI ni MABAVU
MABAVU yakifurika, hakuna ya kuzuia
HAKI ina zikwa
UTU una zama
REHEMA inaibika
HURUMA inayeyuka
UBABE unatamba
UNYAMA unafarajika.
Kujipendekeza ni taaluma ya kipekee
Inahitaji ujasiri wa aina yake
Mazoea ya hali ya juu
Kurudiarudia jina la bosi
Kumsifu bila ukomo.
Uweke uhalisia kando
Utafune ukweli, utapike uongo
Uwe mnafiki, ukandamize nafsi.
Naam, kujipendekeza ni taaluma.
Issa Bin Mariam
11/06/2003
mara nalia
mara nacheka
mara nahuzunika
mara nafarajika
mara naota
mara nawaza
mara nafurahi
mara najuta
mara nashangiliwa
mara nazomewa
wahenga mnisaidie
niko wapi, nchi gani
baharini au barani
ardhini au mbinguni
wahenga mnieleze
nasumbuliwa na nani
majambazi au majamedari?
#Ngorongoro
Itakuwa vema kwa Wizara husika kusitisha mchakato wa kuwahamisha wakazi wa Ngorongoro kuepuka madhara yanayoweza kutokea kijamii, kisiasa na kimazingira. Hakunabudi kukaa na kuwashirikisha wakazi wenyewe, kijiji hadi kijiji kupata maoni yao, hoja zao, manunguniko yao.
I sincerely apologize. I’m wrong. Sub-section 3 of Act seems to say that if the appt authority doesn’t want to renew he has to follow the procedure of 144(3) of const.This means renewal is automatic unless CAG is disqualified by age. My apologies. I overlooked ss (3).
reading together const&law:(1)CAG’s term of office is fixed
@5
yrs.he’s eligible for renewal but appt authority not compelled to do so.(2)If he reaches 65 b4 expiry of 5 yr term, he has to vacate office.(3)appt authority cannot remove him b4 5 yr or age 65 whichever is applicable.
“Chama cha kijamaa kama CCM ni chombo cha uongozi, si chombo cha amri na utawala wa mabavu. Kinaongoza kwa kuelimisha, kuelewesha, kushiriki, kushawishi, kushirikisha na kuelekeza na nguvu yake kubwa inatokana na kukubalika kwake na umma, ... “ Mwongozo wa CCM,1981,uk 40,ibara 53
Kuna lugha na lugha
Lugha ya kutusi
Lugha ya kusifu
Lugha ya kupendeza
Lugha ya kujipendekeza
Lugha ya kuimba
Lugha ya kuvinda
Lugha ya kuchambua
Lugha ya kutumbua
Lugha ya kifumbo
Lugha ya kitumbo
Lugha ya kufarajisha
Lugha ya kutisha
Mfumbo unakufikirisha
Tumbo inakudhalalisha
Njoo 2019 njoo
Uhuru kolea
Haki tandia
Usawa karibia
Ubaguzi torokea
Udikteta fokea
Demokrasia furahia
***
Nawatakia kila la heri
Muepuke na shari
Furahieni samaki ya bahari
Ya nini kutamani kontena ya bandari?
***
Issa Bin Mariam anawaombea
Afya jema
Usomaji mwema
Angalia, tafakari, chambua undani wake na sambaza. Absolutely fantastic. Ujumuisho juu ya uhusiano wa Uhuru wa binadamu na maendeleo yake hauna kifani.
Read politicians’ autobio with a pinch of salt. They’re often self-justifications. Mwalimu didn’t write one. He didn’t want to judge himself. He left it to the posterity. He only wished they would be fair. Intellectual that he was, I guess, he wouldn’t have liked a hagiography.
LIVING AS REBELLION
What do I write,when writing is a curse
What do I speak,when speaking is a scourge
What do I sing,when singing is a sin
What do I think,when thinking is censored!
Why do I live,if living is fearful.
I live to rebel and rebel to live.
Afrika,Mamang’u Afrika
Unadhalilishwa kila dakika
Unakashifiwa kila siku
Ninahuzunika, nina sononeka
Ujasiri ninao
Ari ninayo, nia ninayo
Uwezo sina
Nimeachwa upweke
Wenzangu wamesalimu amri
Marafiki wamenisaliti
Ukimya umetanda, hofu umetawala
Mwanga umejificha
Giza limefichuka
MheZitto. Hotuba yako Bungeni imetufarajisha sana, sisi wana wa Tanzania tuliyolelewa na Mwalimu Nyerere. Tulifundishwa kuthamani utu sio kitu, kusimama pamoja na wanyonge popote pale walipo na kutokuuza heshima zetu kwa uchu wa visenti. Umelinda utu na heshima zetu. Shukran.
Maandamano ya amani kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina - marufuku!
Mbio za mshikamano - marufuku!
Ubebaji wa bendera ya Palestina - marufuku!
Sasa pigeni marufuku hisia na fikra zetu za utu na ubinadamu na binadadamu wenzetu!!
TAFAKURI YA LEO (29/06/2022)
‘Utawala wa Sheria’ ina thamani gani kama utawala wenyewe unavunja sheria na baadai kupitisha sheria nyengine kuhalalisha uvunjaji wake wa sheria?
“Pamoja na kulaani ukatili wa Israel na washirika wake, tunatoa wito kwa Serikali yetu kusimama kidete na kuchukua msimamo thabiti wa kuvunja mahusiano yote na mamlaka katili ya Uzayuni wa Israel.”
HESHIMA KWA VIONGOZI haina maana
UHASAMA KWA WENGI
UZALENDO WA NCHI sio
UTIIFU KWA SERIKALI
UTAWALA WA SHERIA hainmaana
UTELEKEZAJI WA HAKI
UWEZO WAKO WA UAMUZI hm
UBEZAJI WA HAKI YANGU YA KUJIELEZA
NGUVU ZAKO ZA UTAWALA hm
UVUAJI WA UTU WANGU
VITISHO VYAKO si
VIBURUDISHO VYANGU
reading together const&law:(1)CAG’s term of office is fixed
@5
yrs.he’s eligible for renewal but appt authority not compelled to do so.(2)If he reaches 65 b4 expiry of 5 yr term, he has to vacate office.(3)appt authority cannot remove him b4 5 yr or age 65 whichever is applicable.
Rais hana Mamlaka ya Kikatiba kumwondoa CAG kama hajatimiza miaka 65.Sheria ipo wazi. CAG aliyepo madarakani ataondoka kwenye nafasi hiyo iwapo tu ametimiza miaka 65 au utaratibu wa nidhamu umefuatwa.Rais Magufuli amemteua CAG mpya ili kuficha maovu ya Matumizi mabaya Serikalini
Kama huu ndio uchochezi, basi wananchi wengi ni wachochezi.
Huundo wimbo unaotumika kutaka kumuangamiza Vitali Maembe,pamoja na "nyimbo nyingine".
Sambaza Link ya Wimbo huu ili umma uamue kama anastahiki kuhukumiwa au kutuzwa.
#MuachieniVitaliSasa
(1) Lengo haliwezi likawa kujenga uchumi wa viwanda. Lengo liwe kujenga uchumi wa kitaifa utakao simama juu ya miguu miwili - KILIMO na VIWANDA - sekta za uzalishaji ambazo zitegemeane bila kuwa tegemezi. Na kilimo maana yake ni wazalishaji wadogo-wakulima na wafugaji.
Happy birthday Baba yetu, Jemedari wetu
@IssaShivji
MUNGU aendelee kukubariki na kukupa maisha marefu yenye HERI na BARAKA tele
Uendelee kumwaibisha shetani
jiji langu limejaa foleni
kuna foleni na foleni
hospitalini kuna foleni la kutibiwa
chuoni foleni la kuteuliwa
kuna foleni la kutuziwa
foleni la kutimuliwa
matatatizo yamejipanga foleni
matumaini yamejipanga foleni
foleni zinashindana
hakuna mshindi wala mshindwa
sote tumeshindwa
“According to development theories, a country cannot develop without generating debates on how that country can pave the way for its development. One of the main roles of intellectuals in Tanzania is to lead such debates...” Edward Sokoine, 12/10/1983, TAAMULI Vol 13. See below👇
Malenga mashuhuri wa Chile huko Marekani ya Kusini , Pablo Neruda alisema , “Hata kama ukikata maua yote yatachanua upya majira ya vuli “. ( Even if you cut all the flowers , they will bloom again in Spring ).
“The U.S. military emits more carbon than 140 of the world’s individual countries” Pentagon is the single largest institutional consumer of crude oil on the planet.Together,US and UK have around 900 military bases in foreign countries leaving behind carbon imprint.Jan’22, MReview
Ufutaji wa uchifu ulitusaidia sana kujenga umoja wa kitaifa.Nchi zingine Za Afrika (kmNigeria, Ghana nk) wamepata shida kujenga umoja wa kitaifa. Sababu mojawapo ni machifu kulinda himaya zao kwa kukuuza ukabila badala ya utaifa. Tunachotakiwa kusisitiza ni utamaduni wa kitaifa.
I get heartaches witnessing how my country(known for its progressive outlook,&even credited w/ developing an alternative worldview of universal values beyond bourgeois universalism)is fast slipping into racist,sexist,tribalist,religious&homophobic discourse in the public sphere
Taarifa hii ya wawikilishi wa wananchi wa Loliondo wakiwemo Mhe Mbunge, Wah Madiwani, wazee wa mila, ya Mei 2022 haikufanyiwa kazi. Badala yake wakapelekewa jeshi wenye silaha za moto. Hii je ni sawa na haki kwa serikali inayodai kuwa ya wananchi kuwatendea wananchi wake?
trees that are strong&steady
that stand upright&unbending
that weather storms&hurricanes
loggers hate them most
for they need many cuts
from different angles&of varied depths
before they fall
and are chopped off branch by branch
when one of them is felled
indeed it’s a ssad day
umeme umezimika
vikoroboi vimetupwa
vibiriti vimeibiwa
niko gizani
msinipe pole
tupeane pole
nyumba ni ya sote
baba, mama,shangazi, bibi
marafiki na majirani
wabaya na wazuri
viongozi na wafuasi
mapadre na matapeli
tutafutane,tushirikiane
tupeane mawaidha,
tugawane majukumu
Asubuhi mapema
Rafiki yangu kijana mwema
Muuza magazeti
Maisha kustiri
Chini ya kivuli cha mti
Meza ya magazeti kufiti
Mjirani MaNtilie na vyake viti
Kawasha jiko bila kibiriti
Anakata majani mabichi
Kupeperusha bendera kijani
Chaguo ngumu🤷♂️
Raha ya kivuli?
Au Kinga ya kijani?
Wakati gwiji wa Fasihi (RM) anapokutana na chipukizi (IM), ... hata Muonekano ananamisha kichwa kwa haya kana kwamba mwari amekutana na mpenzi wake mara ya kwanza!! 😁😁😁
hoja ni hoja
hoja hugongana na hoja
hoja hujenga mjadala
mijadala hujenga muafaka
hoja ni hoja
hakuna mbadala wa hoja
kinyume cha hoja ni jazba
kinyume cha muafaka ni misuguano
amri haijengi hoja
amri ni hulka ya utumwa
amri ni zao la mabavu
mabavu huzaa uhasama
Kwa wananchi demokrasia = ardhi + ushirikishwaji + Uhuru, haki na uwezo wa kujiamulia mambo yao wenyewe. Mahojiano na Kajubi/Shivji 1992. Does it make sense today?
This morning I came across an absolutely fantastic quote on an old woman’s T-Shirt in a video:
“Prejudice is an emotional commitment to ignorance.” Nathan Rutestian
Picha hii kwangu ni most beautiful picture of the year. Ni ya mwaka. Natamani nione picha kama hii ya vijana wakienda shuleni kila kijiji na kila mji wa nchi yangu kabla sijaitwa mbele ya haki. Kwangu walimu ndio wazalendo!
“When the rulers have already spoken,
Then the ruled will start to speak.
Who dares say ‘never’?
Who’s to blame if oppression remains? We are.
Who can break its thrall? We can.
Whoever has been beaten down must rise up!
Whoever is lost must fight back!”
Bertolt Bretch
Unaweza kulizima wazo-pingamizi kwa mabavu na vitisho lakini kamwe huwezi kulizika. Uhai wa mwili wa binadamu ni chakula; uhai wa bongo la binadamu ni fikra. Fikra hazi shughulikiwi kwa vitisho bali kwa hoja tu.
via
@academia
Power -
-clouds judgement
- deforms discretion
- massages the ego
-robs you of compassion
- breeds contempt for the poor & the powerless
-humiliates humanity
It turns you into a brute
When it abandons you
- you have lost humanity & dignity
- alone and forlorn
- foresaken!
2) Hatimaye korosho zinunuliwe na ushirika wa wakulima wenyewe na kiwanda kimilikiwe na ushirika; ushirika ambao unathibitiwa na wakulima wenyewe. Na hatimaye tuwe na benki ya ushirika ambao utakuwa na hisa za serikali na ushirika. Co-operative benki ndio itakuwa inatoa mikopo.
Tupaze sauti. Utwaaji wa ardhi ya vijiji kiholela au kwa fidia ndogo sio haki wala utu. Taratibu za kisheria na haki za kikatiba lazima zifuatwe. Uwekezaji hauwezi kuhalalisha uvunjaji wa haki za wananchi. Maslahi ya wananchi yana kipaumbele kuliko ya wawekezaji.
Utungo wa kuaaga rafiki yangu wa muda mrefu ulioandikwa mwaka jana (Septemba 28, 2018) kimechapishwa ktk Kitabu ‘Poems for the Penniless’, Mei mwaka huu (2019)
1. There is so much utterly irrational demagoguery, so much empty sloganeering, so much clowning and so much misogynist prejudice - YET all of it goes unchallenged - without even a whimper of disagreement.
Ukimya ukimya ukimya
Ukimya umetanda
Kwa nini nalalamika
Kwa nini nasononeka
Kwa nini?
Ya nini kulalamika
Ya nini kusononeka
Ya nini?
Kwani nina haki?
Ukimya huu
Ni kama ‘black hole’
Hauingiki, hautokeki
Kwa mbali unakushawishi
Ukikaribia unakumeza!
Issa bin Mariam
12/04/2019
END OF YEAR TWEET AND WISH FOR NEW YEAR
What exercise is to body, expression is to thought. Just as body becomes flabby without exercise, so thought becomes fuzzy without expression. Freedom of thought is meaningless without freedom of expression.
The settler colony, Israel, is massacring Gazans with impunity shielded by another powerful settler colony, US. Just as settlers in the US almost wiped off original inhabitants (so-called Indians)from the face of the earth, so are Zionist settlers bent on wiping off Palestinians.
Kila mara nikisikia neno “private sector” (sekta binafsi), najiuliza: Kwani wakulima na wafugaji sio private sector? Sote tunajua wanaotumia neno hilo hawamaanishi wakulima/wafugaji. Wanachomaanisha ni wawekezaji, sio wazalishaji.
This is what made Mwalimu different. Mwl was secure in his intellectual prowess and therefore did not feel threatened by intellectual critiques. Source of this 👇 is: Chemchemi, April 2010, issue no 3. Chemchemi was published by Mwalimu Nyerere Chair in PanAfrican Studies, UDSM.
Vijana wa nyakati zetu hatukuwa na identity crisis. Hatukuwa na mashaka na ubinadamu wetu na hatukutilia shaka uzalendo wetu uliojikita kwenye kusimamia/kutetea haki/maslahi ya wavujajasho. Hatukuwa na haja ya kuimba uzalendo au kupeperusha bendera. Ah! Kila zama na kitabu chake!
ninachukua nafasi hii
bila kupewa
ninatumia kisingizio cha mwaka mpya
bila kuficha
kuwatakia kila la heri
maisha mema yenye afia na maadili
maisha ya mapambano
mapambano ya kujenga
jamii bora
jamii yenye haki
jamii yasiyo na dhulma
jamii ya usawa, ubinadamu na utu
Alamsik
Huko nje wanatamba na economic DIPLOMACY;nyumbani wanafanya economic DESTRUCTION ya wavujajasho. Maswali:(1) Kwanini vijana wa 14-25 wanahamia mijini. Sababu vijijini wamekosa ardhi; ardhi wanapewa wawekezaji. kilimo hakilipi kwa sababu wakulima wananyonywa kupita kiasi.
Bomoa bomoa ya vibanda vya wamachinga wa Vingunguti ni UNYAMA usiomithilika unaofanywa na Mamlaka za Mkoa wa DSM/Wilaya ya Ilala dhidi ya wavujajasho. Mkiti wa Wamachinga Vingunguti amedai kuwa watu wawili wanasemekana kufariki kutokana na kupoteza mali zao. Naulaani unyama huu.
Mwalimu alituasa wakombozi wa wakulima na wafanyakazi ni wao wenyewe. Sasa tunahubiriwa wakombozi wa Tanzania (neno wakulima-wafanyakazi limefutwa) ni wawekezaji. Sasa swali langu, mimi mwanafunzi makini, ni: je wavujajasho watakuwa wanafanya shughuli gani wakati wanakombolewa?