Baraza la Mitihani la Tanzania linatarajia kutangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) 2022 leo tarehe 29 Januari, 2023. Matangazo hayo yatakuwa mubashara (live) kupitia youtube channel ya NECTA (nectaonline) kuanzia saa 4 asubuhi.
Katibu Mtendaji wa NECTA kesho tarehe 07/01/2024 atatangaza matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne na Kidato cha Pili mwaka 2023. Matangazo hayo yatarushwa mubashara (live) kupitia YouTube ya NECTA (Necta Online) kuanzia saa 7:00 mchana.
Baraza la Mitihani la Tanzania limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne na Maarifa (QT) 2022 leo tarehe 29/01/2023. Matokeo hayo yanapatikana kwenye tovuti ya NECTA.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania leo tarehe 23 Novemba, 2023 atatangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2023. Matangazo hayo yatarushwa mubashara (live) kupitia YouTube ya NECTA (Necta online) kuanzia saa 5:00 asubuhi.
Baraza la Mitihani la Tanzania linatarajia kutangaza matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne na Kidato cha Pili 2022 leo tarehe 4/01/2023. Matangazo hayo yatarushwa (Live) kupitia youtube ya nectaonline kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Charles Msonde anatangaza matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, Maarifa (QT) na Upimaji wa Darasa la Nne na Kidato cha Pili iliyofanyika 2019 sasa hivi. Baada ya muda mfupi matokeo hayo yatapatikana kwenye tovuti ya NECTA.
Baraza la Mitihani la Tanzania leo tarehe 15/1/2022 linatarajia kutangaza matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne, Kidato cha Pili na Mtihani wa Kidato cha Nne 2022. Unaweza kutazama tukio hilo kupitia youtube channel ya NECTA (Nectaonline) kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Baraza la Mitihani la Tanzania limetangaza matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne na Kidato cha Pili 2022. Matokeo hayo yanapatikana kwenye tovuti ya NECTA.
Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt. Said A. Mohamed leo tarehe 7/01/2024 ametangaza matokeo ya Darasa la Nne na Kidato cha Pili 2023. Matokeo hayo yanapatikana kwenye tovuti ya NECTA:
Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt. Said A Mohamed leo tarehe 25/01/2024 ametangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) 2023. Matokeo hayo yanapatikana kwenye tovuti ya NECTA.
Baraza la Mitihani la Tanzania linatarajia kutangaza matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu 2023 leo tarehe 13/07/2023. Matangazo hayo yatarushwa live kupitia youtube ya NECTA (Nectaonline) kuanzia saa 6:45 mchana.
Baraza la Mitihani la Tanzania leo tarehe 15/01/2022 limetangaza matokeo ya Upimaji wa Darasa la Nne, Kidato cha Pili na Mtihani Kidato cha Nne. Matokeo hayo yanapatikana kwenye tovuti ya NECTA.
Afisa wa Baraza la Mitihani la Tanzania Ndg. John Duah akiwaeleza wanachuo wa Chuo cha Ualimu Kigogo (DSM) jinsi mfumo wa Usahihishaji wa Kidigitali (Electronic Marking) unavyofanya kazi walipotembelea banda la NECTA kwenye Maonesho ya Sabasaba, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa WyEST Prof. Carolyne Nombo amekabidhi magari 3 kwa Taasisi 3 zilizopo chini ya WyEST ambazo zinatekeleza mradi wa BOOST. Lengo la kupewa magari hayo ni kuongeza ufanisi katika kipindi cha utekelezaji wa Mradi huo. Miongoni mwa Taasisi hizo ni pamoja na NECTA.
Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakisikiliza uwasilishwaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo leo 7 Mei, 2024.
Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt. Said A. Mohamed akitoa taarifa ya maandalizi ya mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu itakayofanyika tarehe 2 hadi 22 Mei, 2023
Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt. Said A. Mohamed leo tarehe 8/4/2024 amefungua mkutano wa Jukwaa la Utafiti la Umoja wa Mabaraza ya Mitihani ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika (Southern Africa Association for Educational Assessment Research Forum) Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Tume ya Mapitio ya Sera ya Elimu kutoka Jamhuri ya Uganda ilifanya ziara katika ofisi ya NECTA Dar es Salaam tarehe 23/04/2024 kujifunza kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 pamoja na Mitaala Mipya na uendeshaji wa Mitihani ya Kitaifa.
UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA NECTA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda leo tarehe 30/11/2023 amezindua rasmi Maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
Baraza la Mitihani la Tanzania leo tarehe 15/01/2021 litatangaza matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne, Kidato cha Pili na matokeo ya Kidato cha Nne 2020.
Baraza la Mitihani la Tanzania leo tarehe 5/07/2022 limetangaza matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu 2022. Matokeo hayo yanapatikana kwenye tovuti ya NECTA.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano Mazingira Dkt. Selemani Jafo wametembelea banda la Baraza la Mitihani la Tanzania na kuona jinsi gani mfumo wa kusahihisha mitihani kidigitali (E-Marking) unavyofanya kazi.
Baraza linapenda kuwajulisha kwamba ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2020 inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mtihani wa Kidato cha Sita umpangwa kufanyika kuanzia tarehe 9/10/2020 hadi 23/10/2020 ni ya Uongo. Hadi sasa ratiba ya mtihani huo bado haijatoka.
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya NECTA katika Ofisi ya Baraza la Mitihani la Tanzania, Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo (katikati) afanya ziara katika Ofisi za Baraza la Mitihani la Tanzania zilizopo Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa amenyanyua juu tuzo ya shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Kilele cha Maadhimisho Miaka 50 ya NECTA yaliyofanyika leo tarehe 16/12/2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali - Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa ametembelea banda la NECTA kwenye Maonesho ya Pili ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid-Arusha.